Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya Umma ya Lebanon katika tamko lake imetoa mkono wa pole kwa kuuwawa kishahidi Ahmad Ghalib Al-Rahwi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Yemen, pamoja na idadi ya mawaziri wa nchi hiyo ambao walipata shahada kufuatia shambulio la ndege za kivita la kihaini la Kizayuni lililowalenga Alhamisi iliyopita katika Barabara ya Quds.
Harakati hiyo imeashiria kuwa tendo hili la kihalifu na la usaliti ni ukiukwaji wa wazi wa mamlaka ya nchi za Kiarabu na ni jinai kubwa inayoongezeka katika orodha ya mashambulio ya kimsingi ya Kizayuni dhidi ya mataifa ya Kiarabu.
Harakati ya Umma imesisitiza kuwa damu ya mashahidi shujaa waliopaa mbinguni katika ardhi safi ya Yemen imeungana na damu ya mashahidi wa umma katika vita vya Tufanu-l-Aqsa, jambo ambalo kwa hakika linaonyesha mapambano ya pamoja katika kuutetea mradi wa Palestina.
Mwisho wa tamko lake, Harakati ya Umma imesema: Kujitolea kunakoshuhudiwa Yemen ni kielelezo cha kweli cha umoja wa umma wa Kiarabu na Kiislamu na ni mwendelezo wa jihadi dhidi ya adui wa Kizayuni ambaye anachukuliwa kuwa tishio la kweli kwa umma wetu wa Kiarabu.
Maoni yako